Deuteronomy 33

Musa Anayabariki Makabila

1 aHii ndiyo baraka Musa mtu wa Mungu aliyotamka kwa Waisraeli kabla ya kifo chake. 2 bAlisema: Bwana alikuja kutoka Mlima Sinai,
akachomoza kama jua juu yao
kutoka Mlima Seiri,
akaangaza kutoka Mlima Parani.
Alikuja pamoja na watakatifu makumi elfu
kutoka kusini,
kutoka materemko ya mlima wake.

3 cHakika ni wewe ambaye huwapenda watu,
watakatifu wako wote wamo mkononi mwako.
Miguuni pako wote wanasujudu
na kutoka kwako wanapokea mafundisho,

4 dsheria ile Musa aliyotupa sisi,
tulio milki ya kusanyiko la Yakobo.

5 eAlikuwa mfalme juu ya Yeshuruni
Yeshuruni maana yake ni Yeye aliye mnyofu, yaani Israeli.

wakati viongozi wa watu walipokusanyika,
pamoja na makabila ya Israeli.


6 g“Reubeni na aishi, asife,
wala watu wake wasiwe wachache.”

7Akasema hili kuhusu Yuda: “Ee Bwana, sikia kilio cha Yuda,
mlete kwa watu wake.
Kwa mikono yake mwenyewe hujitetea.
Naam, uwe msaada wake
dhidi ya adui zake!”

8 hKuhusu Lawi alisema: “Thumimu yako na Urimu
Thumimu na Urimu maana yake Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha kifuani cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.
yako ulimpa,
mtu yule uliyemfadhili.
Ulimjaribu huko Masa
na kushindana naye
kwenye maji ya Meriba.

9 jAlinena hivi kuhusu baba yake na mama yake,
‘Mimi siwahitaji kamwe.’
Akawasahau jamaa zake,
asiwatambue hata watoto wake,
lakini akaliangalia neno lako
na kulilinda Agano lako.

10 kHumfundisha Yakobo mausia yako
na Israeli sheria yako.
Hufukiza uvumba mbele zako
na sadaka nzima za kuteketezwa
juu ya madhabahu yako.

11 lEe Bwana, bariki ustadi wake wote,
nawe upendezwe na kazi ya mikono yake.
Vipige viuno vya wale wainukao dhidi yake;
wapige adui zake hata wasiinuke tena.”

12 mKuhusu Benyamini akasema: “Mwache mpenzi wa Bwana
apumzike salama kwake,
kwa maana humkinga mchana kutwa,
na yule Bwana ampendaye
hupumzika kati ya mabega yake.”

13 nKuhusu Yusufu akasema: Bwana na aibariki nchi yake
kwa umande wa thamani
kutoka mbinguni juu,
na vilindi vya maji
vilivyotulia chini;

14 pamoja na vitu vilivyo bora sana
viletwavyo na jua,
na vitu vizuri sana vinavyoweza
kutolewa na mwezi;

15 opamoja na zawadi bora sana
za milima ya zamani
na kwa wingi wa baraka
za vilima vya milele;

16 ppamoja na baraka nzuri mno
za ardhi na ukamilifu wake,
na upendeleo wake yeye
aliyeishi kwenye kichaka
kilichokuwa kinawaka moto.
Hivi vyote na vikae juu ya kichwa cha Yusufu,
juu ya paji la uso la aliye mkuu
miongoni mwa ndugu zake.

17 qKatika fahari yeye ni kama fahali mzaliwa wa kwanza;
pembe zake ni pembe za nyati,
na kwa pembe hizo atapiga mataifa,
hata yaliyo miisho ya dunia.
Hivyo ndivyo yalivyo makumi elfu ya Efraimu;
hivyo ndivyo yalivyo maelfu ya Manase.”

18 rKuhusu Zabuloni akasema: “Shangilia, Zabuloni, wakati wa kutoka nje,
nawe Isakari, katika mahema yako.

19 sWatawaita mataifa kwenye mlima,
na huko mtatoa dhabihu za haki;
watajifurahisha kwa wingi uliojaza bahari,
kwa hazina zilizofichwa mchangani.”

20 tKuhusu Gadi akasema: “Atabarikiwa yeye aongezaye milki ya Gadi!
Gadi huishi huko kama simba,
akirarua kwenye mkono au kichwa.

21 uAlijichagulia nchi nzuri kuliko zote
kwa ajili yake mwenyewe;
fungu la kiongozi lilikuwa limehifadhiwa
kwa ajili yake.
Viongozi wa watu walipokusanyika,
alitimiza haki ya mapenzi ya Bwana,
na hukumu zake kuhusu Israeli.”

22 vKuhusu Dani akasema: “Dani ni mwana simba,
akiruka kutoka Bashani.”

23 wKuhusu Naftali akasema: “Naftali amejaa tele upendeleo wa Bwana,
naye amejaa baraka yake;
atarithi magharibi na kusini.”

24 xKuhusu Asheri akasema: “Aliyebarikiwa zaidi sana katika wana ni Asheri;
yeye na apate upendeleo kwa ndugu zake,
yeye na anawe miguu yake kwenye mafuta.

25 yMakomeo ya malango yako yawe chuma na shaba,
nazo nguvu zako zitakuwa sawa na siku zako.


26 z“Hakuna mwingine kama Mungu wa Yeshuruni,
ambaye hupanda juu ya mbingu ili akusaidie,
na juu ya mawingu katika utukufu wake.

27 aaMungu wa milele ni kimbilio lako,
na chini kuna mikono ya milele.
Atamfukuza adui yako mbele yako,
akisema, ‘Mwangamize yeye!’

28 abHivyo Israeli ataishi salama peke yake.
Mzao wa Yakobo ni salama
katika nchi ya nafaka na divai mpya,
mahali ambapo mbingu
hudondosha umande.

29 acEe Israeli, wewe umebarikiwa!
Ni nani kama wewe,
taifa lililookolewa na Bwana?
Yeye ni ngao yako na msaada wako,
na upanga wako uliotukuka.
Adui zako watatetemeka mbele yako,
nawe utapakanyaga
mahali pao pa juu.”
Utapakanyaga mahali pao pa juu maana yake mtakanyaga juu ya miili yao.

Copyright information for SwhKC